Auwa watoto wake wawili na mwenyewe kujinyonga sababu hii - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 16 September 2018

Auwa watoto wake wawili na mwenyewe kujinyonga sababu hii


Dotusi Isaya ambaye ni Mkazi wa Chanika jijini Dar es salaam, anadaiwa kuwaua watoto wake wawili na kumjeruhi kwa panga mkewe pamoja na mama mkwe, kisha kujiua baada ya kukataliwa kuwachukua wanae.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pudensiana Protas, akizungumzia tukio hilo amesema Isaya alifanya mauaji hayo usiku wa kuamkia jana huko Nachingwea mkoani humo ambapo mtuhumiwa alikwenda Nachingwea anakoishi mkewe Mariam Lucas na kujificha pembeni mwa nyumba ambayo haijamaliza kujengwa (pagala) akimvizia kisha kumkata panga eneo la kisogo na begani.

“Baada ya kumkata mkewe aliingia ndani ya nyumba (katika) chumba wanacholala watoto na kukuta wanawe wawili wamelala na watoto wengine, lakini yeye aliwaua wanawe kwa kuwakatakata”, amesema Kamanda.

Kamanda amesema kuwa Isaya ameamua kufanya tukio hilo baada ya mkewe kumkatalia asiende na watoto wake Bukoba baada ya kuondoka jijini Dar es salaam walikokuwa wakiishi awali, ambapo mke wake alimwambia mume wake kuwa watoto wakiwa wakubwa atawachukua, lakini kwa sasa ataendelea kuishi nao kwa kuwa bado ni wadogo.

Kamanda ameongeza kuwa kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamesema walianza kusikia vilio saa sita usiku na walipofika eneo la tukio waliwakuta majeruhi wawili (Amanda na Mariam) pamoja na maiti za watoto wawili pamoja na mtuhumiwa akiwa amejinyonga.

No comments:

Post a Comment