Apple kuzindua matoleo matatu mapya ya iPhones kesho, waiga teknolojia ya Huawei na Samsung - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 11 September 2018

Apple kuzindua matoleo matatu mapya ya iPhones kesho, waiga teknolojia ya Huawei na Samsung

Kesho kampuni ya Apple itakuwa na mkutano mkubwa nchini Marekani ambapo inatarajia kuzindua matoleo mapya ya simu zake iPhones, Saa Janja (Apple Watch Series 4) na iPad Pro.
Kwenye matoleo mapya ya iPhone itakuwa ni series ya iPhone X’s ambapo matoleo matatu ya iPhone XS, XS Plus na toleo jipya la iPhone XC ambalo ndio toleo litakalouzwa kwa bei ndogo zaidi ya yote, simu hiyo itauzwa dola $699 sawa na Tsh Milioni 1.5, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa 9to5Mac .
Matoleo mengine ya iPhone XS Plus na XS yatauzwa kwa dola $1000 na dola $900, ambazo sawa na Milioni 2.2 na Milion 2 kwa kila moja kwa pesa za madafu.
Kikubwa zaidi ni kwamba matoleo hayo yatakuja na teknolojia ya laini mbili (Dual SIM Card) kama zilivyo simu za makampuni mengine kama Huawei na Samsung, hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizovujishwa na mtandao wa simu za mikononi wa China Telecom wa nchini China.


Hata hivyo, mtandao huo haujaeleza kama matoleo yote ya iPhone X’s kama yatakuwa na laini mbili. Uzinduzi huo utafanyika kesho Jumatano Septemba 12, 2018 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na utakuwa Live kupitia ukurasa wa Twitter wa Apple.

No comments:

Post a Comment