ZSSF YATOWA MAFUNZO KWA WAFANYA KAZI WANAOTARAJIWA KUSTAAFU. - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 16 August 2018

ZSSF YATOWA MAFUNZO KWA WAFANYA KAZI WANAOTARAJIWA KUSTAAFU.

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Khamis Mussa Omar amewataka wastaafu kujitayarisha wakati wa kukaribia kustaafu na kujipanga vizuri kimaisha ili kuepuka baadhi ya matatizo yasiyokuwa ya lazima.
Hayo aliyasema wakati akifunguwa mafunzo ya mara ya kwanza kwa wastaafu watarajia yaliyotayarishwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) yaliyofanyika  Ukumbi wa mkutano wa Kariakoo Mjini Zanzibar.
Alisema kuwa kustaafu nijambo kubwa ambalo linahitaji mtu kujitayarisha vizuri anapokaribia kustaafu ili kujiimarisha katika mpangilio wake wa kimaisha  wakati wa kustaafu.
Aidha alisema wastaafu wengi huonekanwa kuanguka kimaisha mara baada ya kustaafu kutokana na kutojiandaa vizuri wakati wa utendaji wao kazi jambo ambalo linawafanya kupata  mawazo yanayopelekea maradhi.
“Wastaafu wengi huwa hawajiandai kimaisha kabla ya kustaafu hivyo husababisha kupata maradhi mbali mbali kitu ambacho kinapelekea mfumo mbaya katika maisha yao“alisema Katibu Mkuu huyo.
Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafahamu matatizo yanayowakabili wastaafu hivyo watahakikisha kuyatatua matatizo hayo katika kuwajengeya maisha yaliyobora.
Pia alisema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha wastaafu wanapata haki zao kwa wakati na kuimarisha mazingira mazuri ya kustaafu ili kutimiza malengo waliyojiekea.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) Sabra Issa Machano alisema kuwa (ZSSF) imeamua kufanya semina kwa wastaafu ili kuwapa ushauri wa kujiandalia mazingira mazuri  kabla ya kustaafu.
Hata hivyo alisema Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) umetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake hivyo watahakikisha wanachama wa mfuko huo wanapata huduma nzuri kupitia mfuko watakaotumia.
Sambamba na hayo alisema mfuko huo wa ZSSF ni kwa watu wote waliyojiunga hivyo watafanya juhudi mbali mbali katika kazi yao ili kutimiza lengo lilokusudiwa ndani ya mfuko huo.
“Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) ni kwa watu wote waliojiunga hata kwa wajasiria mali mbali mbali hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanatumia mfuko huo ili kuendelsha maisha yao.”alisema Mkurugenzi Mtendaji Sabara.
Mkurugenzi Sabra aliongeza kuwa mfuko huo kwasasa imekuwa hivyo watazidisha juhudi katika huduma zao kwa wahusika kwa kuendelea kuwajali kwa kuwaelekeza vitu mbali mbali ili kuepukana na matatizo  katika maisha yao.
Kwa upande wa mtoa mada Bwana Daudi Mattaka aliweza kuwasilisha mada mbali mbali kwa wastaafu hao ili kuwasaidia wakati wa kustaafu miongoni mwa mada hizo ni ikiwemo utangulizi wa maisha,Maandalizi ya nini kifanyike pamoja na umuhimu wa kujiandaa kabla ya kustaafu.
Pia aliwataka wastaafu hao kuridhika na hali ya kipato walichonacho katika maisha yao ili kuepuka tamaa ambayo itawapelekea kuharibu maisha yao.
Mafunzo hayo ya siku moja ya kuwandaa  wafanya kazi wastafu yameandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na kufadhiliwa na Benki ya NMB na Benki ya TPB. 
Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar  (ZSSF)  Sabra Issa Machano akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Khamis Mussa Omar  ambae ni Mgeni Rasmin katika  ufunguzi wa Mafunzo ya Kwanza kwa Wastaafu watarajiwa yaliyofanyika Ukumbi wa Mkutano   kariakoo Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipaqngo Khamis Mussa Omar akifunguwa Mafunzo ya kwanza kwa Wastaafu watarajiwa yaliyofanika Ukumbi wa  Mkutano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) uliopo Kariyakoo Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wastaafu watarajiwa wakimsikiliza  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar  hayupo pichani wakati wa Uzinduzi wa mafuzo hayo.

Na Maryam Kidiko– Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment