Zari Afanya Kufuru Birthday ya Mwanaye Tiffa - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 6 August 2018

Zari Afanya Kufuru Birthday ya Mwanaye Tiffa

MZAZI mwenzie na mwana-muziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari’ amefanya kufuru ya mwaka baada ya kuandaa bonge la pati ya siku ya kuzaliwa mtoto wake Tiffah Diamond inayosherekewa leo (Jumatatu) huko Pretoria, nchini Afrika Kusini.Mwamama huyo ambaye anaonekana wazi aliipania siku hii ya mtoto wake kwani hapo awali aliandaa watu maalumu wa kumpiga picha mbalimbali akiwa amevalia magauni tofautitofauti huku akiwa amezungukwa na keki nyingi.AONYESHA MAVAZI YA SIKU HIYO

Wiki moja kabla ya sherehe alionyesha pia vitu mbalimbali vikiwemo nguo, viatu na mabegi ya mkononi ambavyo angevaa Tiffah siku ya bethidei yake.

“ Kwa kweli Zari ni kiboko vitu vyote hivyo ni kwa ajili ya sherehe ya mtoto? Hongere zake,” aliandika komenti msichana mmoja kwenye ukurasa wa Instagram ya Zari kulikowekwa picha za maandalizi hayo ya sherehe.
AKODI NDEGE KUTOA MSAADA

Katika kuonesha jeuri ya fedha, Zari alifanya kufuru nyingine kwa kukodi ndege ya kumpeleka nchini Uganda alikokwenda kutoa msaada kwenye kituo cha kulelea watoto wanaoishi mazingira magumu cha Arua.

Yote hayo ni mjumuisho wa mambo yanayoambana na sherehe ya kuzaliwa kwa Tiffah ambaye mwaka huu anatimiza miaka mitatu.

Hata hivyo sherehe hiyo haiivunji ile inayoandaliwa na Diamond iliyopangwa kufanyika Agosti 18, nchini Afrika Kusini huku ikielezwa kuwa itafanyika kwa siku tatu mfululizo na kuwajumuisha wanamuziki maarufu kutoka nchi mbalimbali.Hata hivyo, wengi kati ya watu waliotoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kitendo cha Zari kumfanyia mwanaye bethidei kivyake walisema inawezekana hataki kushirikiana na mzazi mwenzake ambaye ametengana naye.


“Kwa nini asiunganishe sherehe na ile anayofanya Diamond, au ndiyo anamwaga fedha aonekane tajiri,” mchangiaji mmoja aliandika huku wengine wakimponda kwa kumwambia amwache Zari afanye yake na kwamba yeye afe na umaskini wake.

No comments:

Post a Comment