Z Anto kujipima ubavu na wimbo Mpaka Naogopa ‘mimi niwa tofauti na wengine’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 2 August 2018

Z Anto kujipima ubavu na wimbo Mpaka Naogopa ‘mimi niwa tofauti na wengine’

Msanii wa muziki Z Anto ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo kama Mpenzi Jini, Kisiwa cha Malidavi pamoja na nyingine nyingi, anajipanga kuachia wimbo wake wa pili baada ya ukimya wa muda mrefu.
Muimbaji huyo aliambia Bongo5 kwamba wimbo wa kwanza ‘Kacheze Unakochezaga’ ulikuwa wakuombea msamaha kwa watanzania kutokana na ukimya wake na baada ya kuona amekubaliwa anajipanga kuachia wimbo wake mpya alioupachika jina ‘Mpaka Naogopa’.
“Ni project mpya inakuja soon, wimbo nimefanya kwa Mazuu ni ngoma kali sana ambayo itakuja kuwaonyesha mashabiki kwamba mimi ni nani katika muziki wa BongoFleva, nimefanya vingi lakini pia naweza kubadilika,” alisema Z.
“Kacheze Unakochezaga ni wimbo ambao niliuachia kuwaomba mashabiki msamaha baada ya kukaa muda mrefu bila kuachia wimbo. Na wimbo wangu mpya ‘Mpaka Naogopa’ ni wimbo ambao utawafanya mashabiki wangu waamini kwamba Z Anto ni mtu au msanii tofauti sana katika tasnia ya muziki na ni tofauti na hao wengine ndio maana nikasema mimi siji kushindana kwa sababu nina kitu tofauti,”
Muimbaji huyo amedai tayari ameshaanza kufanya maandalizi ya video ya wimbo huo chini ya director Msafiri.
Pia amewataka mashabiki wa muziki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya project zake nyingi kwani ndani tayari amesharekodi nyimbo zaidi ya 20.

No comments:

Post a Comment