YANGA YAWEKA MPUNGA WAKE WA MICHANGO HADHARANI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

YANGA YAWEKA MPUNGA WAKE WA MICHANGO HADHARANI


Na George Mganga

Uongozi wa Yanga umeweka hadharani kiasi cha fedha ilichopokea kutoka kwa wadau wake ambazo ni za mchango kwa ajili ya kuisaidia klabu.

Hivi karibuni Yanga kupitia Kaimu Katibu wake, Omary Kaaya, alitangaza kuanzisha utataribu wa kuichangia klabu ili iweze kuendesha shuguli zake muhimu kutokana na kupitia kipindi cha mpito.

Katika siku nane za mwanzo kuanzia Agosti 2 mpaka 10, Yanga imepokea kiasi cha shilingi za kitanzania 3,073,263.
Hata hivyo mabosi wa Yanga wamezidi kuwaomba wapenzi, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuzidi kuichangia klabu ili iepukana na hali ngumu ambayo inapitia kwa sasa ili mambo yazidi kwenda sawa.

No comments:

Post a Comment