Yanga kupiga kambi Moro - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 2 August 2018

Yanga kupiga kambi Moro

KIKOSI kizima cha Yanga leo kinaelekea Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema atatumia kambi hiyo kuwajenga wachezaji wake 'stamina' pamoja na kuwapa mbinu mbalimbali.

Mratibu wa klabu hiyo, Hafidh Saleh, aliliambia Nipashe kuwa, taratibu za safari hiyo ambayo awali ilikuwa ifanyike juzi zimekamilika.

"Leo (jana) tunafanya mazoezi jioni pale Chuo cha Polisi Kurasini, baada ya hapo kesho (leo) asubuhi tunaelekea Morogoro na kikosi kizima," alisema Saleh.

Alisema kocha wa timu hiyo, Zahera, ameomba kambi hiyo ili kuweza kuwaandaa wachezaji wake vizuri kabla ya kuanza kwa ligi.

"Kimsingi, kocha ameona mapungufu kwa kutazama michezo miwili ya Kombe la Shirikisho tuliyocheza dhidi ya Gor Mahia, hii itakuwa nafasi nzuri kwake kurekebisha mapungufu hayo na kuwapa wachezaji mbinu zake," alisema Saleh.

Alisema wachezaji wote wapya watakuwa sehemu ya kikosi hicho ambacho kitakaa Morogoro kwa zaidi ya wiki mbili.

Yanga itafungua pazia la Ligi Kuu kwa kucheza na Mtibwa Sugar Agosti 23, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment