YANGA KUKIPIGA NA TIMU DARAJA LA PILI KILOMBERO LEO KUPATA KIPIMO CHA KUWAMALIZA WAARABU - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

YANGA KUKIPIGA NA TIMU DARAJA LA PILI KILOMBERO LEO KUPATA KIPIMO CHA KUWAMALIZA WAARABU


Kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Agosti 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga inashuka dimbani kukipiga na Mkamba Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.

Yanga watashuka na dimbani majira ya saa 10 kucheza na Rangers katika Uwanja CCM Mkamba uliopo mjini Kilombero ili kukikipa kikosi kuelekea mechi dhidi ya waarabu.

Uongozi wa Yanga umeamua kukipelekea kikosi Morogoro kwa ajili ya kuongeza zaidi idadi ya wafuasi wake kutokana na kuwa na mashabiki wengi ambao wanaipenda klabu Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema lengo kubwa la kucheza na timu hiyo ya Daraja la Pili ni maandalizi kuelekea mechi na USM Alger ambayo itafanyikia Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment