WILLIAN AFURAHIA BOSS WAKE KUONDOKA CHELSEA - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 16 August 2018

WILLIAN AFURAHIA BOSS WAKE KUONDOKA CHELSEA


Winga wa Chelsea Willian anasema kuwa hakuna sababu ambayo ingemfanya kusalia katika klabu hiyo iwapo aliyekuwa mkufunzi wa klabu hiyo Antonio Conte angeendelea kuwa mkufunzi.

Conte alishinda taji la ligi ya Uingereza 2016-17 lakini akafutwa mwezi Julai baada ya kumaliza katika nafasi ya tano.

Mrithi wake aliyekuwa mkufunzi wa Itali Maurizo Sarr alishinda mechi yake ya kwanza ya ligi baada ya kuilaza Huddersfiedl 3-0 siku ya Jumamosi.

''Meneja anatuambia tucheze tujifurahishe uwanjani'' , Williana alisema. ''Ni raha kucheza hivi , nadhania hivyo''.

''Tuna wachezaji wengi walio na ubora mbele kama vile Eden Hazard na Pedro. Wachezaji kama hao wanataka kucheza. Ndio maana yeye Sarri anataka tucheza mchezo mzuri baada ya kuwasili Cheslea''.

''Hivi ndivyo tutakavyoweza kucheza msimu huu''.

No comments:

Post a Comment