Watu Zaidi ya 35 Wafariki Dunia Baada ya Daraja la Mwendo Kasi Kuvunjika Italia - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

Watu Zaidi ya 35 Wafariki Dunia Baada ya Daraja la Mwendo Kasi Kuvunjika Italia

Kazi ya uokoaji imeendelea kufuatia kuvunjika kwa daraja la barabara ya mwendo kasi huko kaskazini mwa Italia katika mji wa Genoa na kusababisha vifo vya watu wapatao 35.

Picha ya video inaonyesha upande mmoja wa mnara ulisababisha daraja kuanguka kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya. Sauti za kuomba msaada kutoka kwa watu wanaosadikiwa kunaswa katika mabaki ya daraja hilo zimesikika usiku kucha.

Tazama daraja la magari lilivyoanguka na kuuwa watu 30 Itali
Wafanyakazi wa dharura wanajaribu kuwatafuta watu walioanguka na magari yao huku wakiwa wanasaidiana na mbwa wenye utaalamu kwa kunusa .

Waziri wa usafirishaji Danilo Toninelli ameliongelea janga hilo kuwa kubwa na Ufaransa nayo imehaidi kushirikiana pamoja na Italia katika janga hilo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameandika ujumbe wa pole katika ukurasa wake wa Twitter kwa waitaliano na wafaransa pia.

No comments:

Post a Comment