WATANO WAFARIKI AJALINI, DEREVA ATIMUA MBIO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

WATANO WAFARIKI AJALINI, DEREVA ATIMUA MBIO


Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa mkoani Mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Busurwa mwambao wa Ziwa Victoria wilayani Rorya kwenda mjini Tarime kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe amesema ajali hiyo ilitokea katika Kitongoji cha Bukwe eneo la Mika alfajiri ya jana Agosti 14, 2018, ambapo uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni mwendo kasi uliosababishwa na dereva aliyekuwa akiwakimbia askari wa doria.

Kamanda Mwaibambe amesema dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la Athumani Masiaga ambaye ni miongoni mwa waliofariki dunia alikataa kutii amri ya kusimama iliyotolewa na askari wa usalama barabarani kutokana na kubeba samaki wanaosadikiwa kupatikana kutokana na uvuvi haramu.

No comments:

Post a Comment