WASANII WAANGUA VILIO BAADA YA KUONA JENEZA LENYE MWILI WA MZEE MAJUTO, KUZIKWA KESHO - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 9 August 2018

WASANII WAANGUA VILIO BAADA YA KUONA JENEZA LENYE MWILI WA MZEE MAJUTO, KUZIKWA KESHO


Msiba wa msanii mkongwe, Amri Athuman' King Majuto' umewaliza wasanii mbalimbali waliojitokeza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipofia.

Wasanii kadhaa walifika hospitalini hapo kwa ajili ya msiba huo ambao utasafirishwa kwenda Tanga.

Wasanii hao walianza kuangua vilio baada ya kuona jeneza lenye mwili wa mzee Majuto likipitishwa kutoka mochwari.


Tayari imeelezwa, msiba utakuwa kwake Tanga kabla ya kwenda kuzikwa kijijini kwake kesho saa saba mchana.


No comments:

Post a Comment