Wakala wa Pogba atua Uingereza kwa mazungumzo na Man United, Barca na Juve wasubiria majibu - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 6 August 2018

Wakala wa Pogba atua Uingereza kwa mazungumzo na Man United, Barca na Juve wasubiria majibu

Wakala wa mchezaji Paul Pogba ambaye ni Mino Raiola yupo nchini Uingereza kwa mazungumzo na klabu ya Manchester United juu ya uamisho wa kiungo huyo wa Ufaransa.
Klabu ya Barcelona na Juventus zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mshindi huyo wa taji la kombe la dunia, Pogba ambaye siku za hivi karibuni ameonyesha kutokuelewana na meneja wake Jose Mourinho.
Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Raiola yupo Uingereza kwaajili ya kufanya mazungumzo na United juu ya uhamisho wa kiungo huyo wakati dirisha la usajili nchini humo likitarajiwa kufungwa siku ya Alhamisi.
Barcelona inahitaji kujenga muunganiko wa Pogba, Philippe Coutinho na Lionel Messi ili kuhakikisha inaimarisha kikosi chake msimu huu.
Wakati Juventus baada ya kukamilisha dili la Cristiano Ronaldo lenye thamani ya pauni milioni 100 imesema kuwa ipo katika mbio za kumsajili Mfaransa huyo.

No comments:

Post a Comment