Utawala wa kiimla unavyomtesa Martial Old Trafford, Mourinho Anamyanyasa - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 5 August 2018

Utawala wa kiimla unavyomtesa Martial Old Trafford, Mourinho Anamyanyasa

Rafiki mmoja aliniuliza kwanini Man United inacheza soka bovu. Jibu langu lilikuwa rahisi tu “Bodi ya Man United ilikuwa na tamaa ambayo iliponzwa na muda” Bodi ya Man United ilikuwa inamjua vyema kabisa Mourinho. Walikuwa wanajua ni kocha huyu huyu aliyemwagiza mkata uwanja wa Bernabeu aache nyasi ziwe kubwa ili pasi za Barcelona zigome. Ni kocha huyo huyo aliyemtumia Michael Essien kama beki namba 2 na kuwaambia wabrazil kwamba Coentrao ni bora kuliko Marcelo.

Tatizo la bodi ya Man United liliponzwa na mafanikio ya Mourinho aliyopata ndio maana mabosi wa Man United wakamuona Chalton ni mnafiki alipowaeleza kuwa Mourinho hafai Old trafford. Bobby Chalton 2012 aliwaambia Mourinho hafai kuifundisha Man United lakini mwaka 2016 Ed Woodward akamwona Charlton ni mjinga.Kuna baadhi ya tabia za Mou ambazo hazipo sawa. Mourinho ni sawa na baadhi ya viongozi wa Afrika. Wakiona watu wanakwenda kinyume na matakwa yao basi wanawapoteza. Viongozi wa Afrika baadhi yao wanapata uongozi kwa demokrasi lakini wanatawala kwa mabavu. Kwa sasa Mourinho anataka kuendelea kubakia Madarakani. Uongozi wake mbaya anatupia lawama kwa wafuasi wake na viongozi kama alivyosema hivi juzi kuwa Ed Woodward hafuati matakwa yake. Mourinho anapenda kutafuta madaraka/matokeo kwa njia yeyote bila kujali wapiga kura wake wanamwaga damu au lah nikimaanisha kuwa wachezaji wanakosa furaha kwa uchezaji wakeKuna makelele yanapigwa. Kwanini Sanchez alikuja United? Mourinho atawajibu kirahisi Sanchez alipatikana bure. Kuna kosa linakwenda kutendeka tena Old trafford. Kosa la kwanza ni Angel Di Maria kuondoka na sasa Martial.

Mourinho anatawala kiimla. Matatizo ya klabu yake anayaweka kwenye mwili wa mtu mmoja. Martial analalamikiwa kila mara timu inapokosa matokeo chanya. Anakosa hata amani ya kucheza uwanjani kwa uhuru. Martial ameshikiwa mtutu wa bunduki na anacheza kama wapigwa kura wa nchi jirani. Ni martial yule yule waingereza walizunguka barabara ya John Gilbert way wakimwimbia.Kijana huyu mwenye 22 alikuja United mwaka 2015 dakika za mwisho kabisa kwa dau £58m. Monaco wakawaambia United kwamba watahitaji £7.2m kama Martial angetwaa Ballon d’Or kabla ya 2019. Kiwango chake cha msimu mmoja kilimfanya Sir Alex Ferguson anene jambo “he can do anything.” alitabiri kuwa Martial atafanya makubwa. Sina imani kama Mourinho aliwahi kuwa na mshindi wa Ballon d’Or kwenye kikosi chake.Labda Ferguson hakujua kama Mourinho angevaa viatu vyake hapo baadae ndipo akatamka maneno yale. Martial yupo radhi kuondoka Manchester. Ndio. Unadhani Man United ni ukoo? Hapana. Ananyanyasika. Amekosa hata nafasi ya kwenda kuvaa medali ya kombe la dunia. Unahisi moyoni mwake anajisikiaje? Unadhani Martial angekuwa timu inayomwamini na kumwacha acheze huru asingekwenda Urusi?Ni mwaka 2013 Kevin De Bruyne nae aliingia kwenye mkasa kama huu. Kocha wa Chelsea alikuwa Jose Mourinho, alimruhusu kijana mwenye 22 kuondoka kwa fedheha. Mourinho alikerwa na kiwango chake na kusema hachezi kea kujituma. Akadai yeye kuwa KDB alikuwa mvivu. Akaongea kwa nyodo sana mara baada ya mchezo wao wa kombe la ligi [League Cup] dhidi ya Swindon“Kevin anapaswa kuelewa kwamba Chelsea sio Werder Bremen, unapaswa kupambana kwa kujitoa sio kwenye mazoezi sio mechi. Mchezo unaokuja ni wa mwisho kwake anapaswa kujua hilo kama hatabadilisha tabia yake” Alisema Mourinho

Uzuri ni kwamba De Bruyne sio kama Martial. Martial ni kama bubu. Muda wote ametulia. KDB wala hakuvumilia hata kidogo kauli ya mkufunzi wake, kesho yake alimfuata na kumwambia “naondoka”. Walikutana kwenye korido, Mouringo alishtuka sana kumuona KDB katika sura ile. Alizoea kwamba KDB sio muongeaji sana“Nilijituma sana na nilipambana mno, nilipoteza takribani kilo 4 mpaka 5. Nilikonda hata daktari aliniuliza vipi mbona umepungua hivi. Ndugu, jamaa na marafiki walinishangaa. Lakini kuna mtu akawa hanielewi. Nilimfuata tu kirafiki na kumwambia niache niende”

“Mwanzoni Mourinho akajifanya kukataa, “nilijua tu alikataa kinafiki” alitaka kujisafisha mbele za watu. Akanifuata usiku kwenye chumba changu. Alinikuta na wachezaji wengine akaniita, nikamfuta mpaka kwenye bustani, alikuja kwa hamaki sana na alikuwa kama hajiamini”“Nikamuuliza mwalimu vipi umeshapata klabu ya mimi kwenda? Sitaki kuondoka kwa mkopo nataka kuondoka kabisa. Akasita akam sekudne kadhaa akaniambia pambana utapata nafasi, nikamwambia nishafanya maamuzi huwezi kunibadilisha maana nitacheza kwa presha kubwa, niache niende.” Alisema Kevin De bruyne.

Hivi majuzi tumepata fununu Mourinho ameruhusu Martial aondoke. Ni siku kadhaa baada ya bodi kumkabidhi mkataba mpya Martial ila aliukataa. Unajiuliza wakati wanajadili mkataba huo Mourinho si alikuwepo? Kwanini Mourinho aliruhusu bodi iandae mkataba mpya wakati anajua hakumhitaji? Mchezaji wa kiwango kikubwa anapokuwa hachezeshwi ni wazi kuwa mwalimu hamtaki na ndivyo ilivyokuwa kwa Martial na Mourinho.Kikao cha mwisho cha mabosi wa united kimekubaliana kwamba Martial asiondoke. Wanakumbuka waliyofanya kwa Paul Pogba. Kuna wakati timu haipaswi kumsikiliza mwalimu pekee. Avran Glazzer huenda sio mfuatiliaji sana wa mpira lakini Ed Woodward sio kwamba hawasikii akina Scholes wanachoongelea kuhusu mfumo wa Mourinho.

Ni dunia hii hii Mourinho anapigania Fellain kuongezewa mkataba na kumataa Martial. Yule Salah aliyemkataa amefunga mabao 43 kwenhe michezo 49 kwa Liverpool. Unadhani Roman Abramovic anajisikiaje anapomuoma Morata akihangaika kama kuku aliyesahau sehemu aliyotagia huku Salah akiwania Ballon d’Or.Nani asiyejua mashabiki wa Man United wanapenda mpira wa kushambulia? Mourinho anacheza vipi? Katika mfumo huu Martial ameanza asilimia 46 tu ya mechi zote tokea Mourinho atue 2016. Ni mchezaj yule yule ambaye msimu wa kwanza alifunga mabao 17 na kuanza mechi kwa asilimia 85 chini ya Lois Van Gaal. Hata hivyo licha ya Martial kuanzia benchi hakuna mshambuliaji wa Man united aliyemzidi kwa mabao ispokuwa Lukaku. Je huyu Mourinho kama sio Idd Amini ni nani?Muda sio mrefu jukwaa la Stretford Enders litaanza kubeba mabango ya kumtaka Mou aondoke.


Mimi ni Privaldinho (Instagram)

No comments:

Post a Comment