Uongozi wa WCB Wawazawadia Magari Mboso na Lavalava - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 8 August 2018

Uongozi wa WCB Wawazawadia Magari Mboso na Lavalava

WCB yawanunulia magari wasanii wake, Mbosso na Lavalava hii ni mara baada ya Diamond Platnumz kuposti video clip kwenye Insta Story yake na kuonesha magari hayo hapo jana siku ya Jumanne.

Mara baada ya kukabidhiwa kwa zawadi hiyo ya magari Lavalava amesikika akisema ”Ebwana eeh kama unavyoona mambo yamefana, bwana tukutane sheli muambie na mwenzako, mr Mbosso muambie wasikie asiyefanya kazi na asile,” amesema Lavalava.

Wakati kwa upande wake Mbosso amewaambia mashabiki zake kuwa ” Ebwana eeh kesho tukutane Wasafi tv.”

Magari hayo waliyopewa wasanii hao wawili ni aina ya Toyota Harrier moja nyeusi na nyingine rangi ya maziwa huku mashabiki wa muziki wakiwa wanatamani kujua kuhusu wasanii wengine wa WCB kupata kwa zawadi hizo.

Wasanii hawa wawili wamepishana mwaka moja tu kujiunga kwao na WCB wakati Lavalava akitambulishwa May 23, 2017 huku Mbosso kwa upande wake akitangazwa rasmi January 27, 2018.

No comments:

Post a Comment