UJUMBE WA UMOJA WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU (UAE) WAWASILI ZANZIBAR - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 9 August 2018

UJUMBE WA UMOJA WA NCHI ZA FALME ZA KIARABU (UAE) WAWASILI ZANZIBAR

Ujumbe wa timu ya Wataalam 16 wa Umoja wa Nchi za Umoja wa Falme ya Kiarabu (UAE) walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo ,ujumbe huo Umekuja kufuatilia makubaliano ya Ziara ya Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Nchi za UAE. aliyoifanya mwanzoni  mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 08/08/2018.
Mshauri  wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uchumi na Fedha na Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa  akisalimiana na Ujumbe wa timu ya Wataalamu 16 kutoka Nchi za Umoja wa Falme ya Kiarabu (UAE) ulipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,kufuatia  Ziara ya Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Nchi za UAE. aliyoifanya mwanzoni  mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 08/08/2018.
Mshauri  wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uchumi na Fedha na Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa  akisalimiana na Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Najla Al- Kaabi akiongoza  Ujumbe wa timu ya Wataalamu  kutoka Nchi za Umoja wa Falme ya Kiarabu (UAE) ulipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,kufuatia  Ziara ya Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Nchi za UAE. aliyoifanya mwanzoni  mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 08/08/2018.
Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Najla Al- Kaabi (katikati) alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbali mbali akiwa na  Ujumbe wa timu ya Wataalamu  kutoka Nchi za Umoja wa Falme ya Kiarabu (UAE) ulipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,kufuatia  Ziara ya Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Nchi za UAE. aliyoifanya mwanzoni  mwa mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 08/08/2018.

UJUMBE wa timu ya Wataalamu kutoka Serikali ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umewasili nchini leo kwa ziara maalum ya siku nne kwa lengo la utekelezaji yaliokubaliwa katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliyoifanya mwezi Januari mwaka huu katika nchi hizo.
Ujumbe huo wenye wataalumu 16, ulioongozwa na Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Falme za Kiarabu Najla Al Kaabi uliwasili jioni ya leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kiwanjani hapo mara baada ya mapokezi hayo, Mshauri wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Uchumi Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alisema kuwa ujio huo umekuja kwa lengo la kufuatilia makubaliano yote yaliokubaliwa katika ziara hiyo ambayo Dk. Shein alikutana na viongozi wakuu wa Nchi za UAE.
Balozi Ramia alieleza kuwa ujumbe huo umetangulia leo na kesho Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za UAE Reem Ibrahim Alhashimy, atawasili na kuungana na ujumbe huo ambao utakuwepo Unguja pamoja na kutembelea kisiwani Pemba kwa lengo la kuangalia miradi itakayotekelezwa kisiwani humo.
Akitoa maelezo juu ya ujio wa Timu hiyo ya wataalmu Balozi Ramia alieleza kuwa jumla ya miradi saba ambayo imo katika makubaliano itajadiliwa na kuangaliwa utekelezaji wake ukiwemo mradi wa ukarabati wa Hospitali ya Wete pamoja na ujenzi wa Barabara ya Chake hadi Mkoani kisiwani Pemba.
Aidha, Balozi Ramia alieleza kuwa kwa upande wa Unguja miradi itakayohusika ni mradi wa hospitali ya Binguni, Mradi wa ukarabati wa nyumba za Mji Mkongwe, Miradi miwili ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Barabara ya Fumba-Uwanja wa ndege kuelekea mjini.
Aliongeza kuwa katika Timu hiyo ya wataalamu pia, umo ujumbe kutoka Mfuko wa ‘Khalifa Fund’ ambao shughuli zake kubwa ni kuwasaidia wajasiriamali na wale wanaohitaji misaada ya aina mbali mbali ambapo ujumbe huo utakuwepo nchini kwa muda wa siku nne.
Nae Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Falme za Kiarabu Najla Al Kaabi alipongeza mapokezi makubwa aliyoyapata yeye na ujumbe wake.
Pamoja na hayo, alieleza kuwa Nchi za Umoja wa Falme za Kirabu (UAE) inajivunia uhusiano na ushirikiano madhubuti uliopo kati ya nchi za umoja huo na Zanzibar.
Aidha, alieleza kuwa ziara ya Rais Dk. Shein katika nchi za umoja huo imeweza kutoa fursa mbali mbali katika kuimarisha mashirikiano na uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya pande mbili hizo katika kuendeleza miradi mbali mbali ya kiuchumi na kimaendeleo.

Sambamba na hayo, Najla Al Kaabi alieleza kuwa viongozi wakuu wote wa UAE wanathamini uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Zanzibar na umoja wa nchi hizo ambao wanaamini kuwa kuna kila sababu ya kuimarishwa.

Na Ramadhan Othman Abdalla

No comments:

Post a Comment