TFF Walilaani Jeshi la Polisi kwa Kumpiga Mwandishi wa Habari, Waahidi Kuchukua Hatua za Kisheria - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

TFF Walilaani Jeshi la Polisi kwa Kumpiga Mwandishi wa Habari, Waahidi Kuchukua Hatua za Kisheria

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limedai kuwa limesikitishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi jana Agosti 8, 2018 kumpiga Mwandishi wa Habari za michezo akiwa uwanjani kwenye mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya Asante Kotoko.

Taarifa ya kulaani tukio hilo imetolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo ambaye amesema kuwa watafuatilia kila kitu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment