Steve Nyerere, Cloud Wachafua Hali ya Hewa Msiba wa Mzee Majuto Tanga - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Steve Nyerere, Cloud Wachafua Hali ya Hewa Msiba wa Mzee Majuto Tanga

Baada ya mwili wa Mzee Majuto kuwasili nyumbani kwake Mtaa wa Donge katika jiji la Tanga, ilizuka sintofahamu baada ya wasanii wakiongozwa na Steve Nyerere na Cloud 112 kufanya jambo ambalo familia haikupendezwa nalo.

Tukio hilo lilizua kutoelewana kati ya wasanii waliotoka Dar es Salaam na wenyeji wa eneo hilo, baada ya wasanii hao walipofika kuingia ndani na kusema wanaenda kukagua sehemu ya kuhifadhiwa mwili.

Wenyeji waliona kama wamedharauliwa na kuwauliza inamaana sisi hamtuamini hadi  kufikia hatua ya kukagua sehemu ya kuhifadhi mwili?

Miongoni mwa wasanii waliodai sehemu ikaguliwe ni Steve Nyerere na Cloud ambao  waliwaita askari waliovaa kiraia na kuingia nao ndani.

Mzozo huo ulisababisha mwili utolewe kwa fujo kwenye gari ya kubebea wagonjwa, huku watu wakisukumwa na baadae mlango wa nyumba ya Majuto ukafungwa na watu wakaambiwa wasubiri nje.

Baadhi ya wasanii walifika Tanga kwaajili ya mazishi ni JB, Steve Nyerere, Baba Haji, Shamsa Food, Muhogo Mchungu, Simon Mwakifamba ambaye ni Rais wa Shirikisho la filamu na wasanii wengine walikuwa wametangulia ambao ni Riyama, Nisha, Hamornize na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment