Simon Msuva Awa Lulu, Agombaniwa na Timu za Ulaya - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 5 August 2018

Simon Msuva Awa Lulu, Agombaniwa na Timu za UlayaTIMU nne kutoka nchi za Ulaya zimeonyesha nia yawazi kumuwania mshambuliaji wa Klabu ya Difaa El Jadida, Simon Msuva anayekipiga katika Ligi Kuu ya Morocco.

 

Msuva alijiunga na El Jadida, Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 337 akitokea Yanga ambapo amefanikiwa kuonyesha kiwango kiasi cha kuzishawishi timu nyingine hasa zile za Ulaya.

 

Tangu atue klabuni hapo Msuva amekuwa mchezaji pekee wa kigeni katika timu hiyo aliyetoa msaada mkubwa kwa kuifungia mabao mengi kuanzia kwenye ligi kuu hadi Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kusababisha kuongezeka thamani yake.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, baba mzazi wa Msuva, mzee Happygod Msuva alisema kuwa, kwa sasa mwanaye huyo anafuatiliwa na timu nne zikiwemo za Ulaya na nyingine nchini humo kwa kuhitaji huduma yake lakini dau la El Jadida limekuwa likiwakwamisha.

 

“Kuna timu anaendelea kufanya nazo mazungumzo ambazo zimemfuata Msuva ndani ya Morocco na nje ya Morocco ikiwemo timu kutoka Hispania ili kuweza kumsainisha lakini tatizo kubwa limekuwa kwa klabu yake, lakini siwezi kuziweka wazi hizo timu hadi mipango itakapokamilika.

 

“Al Jadida inahitaji karibu shilingi bilioni 4 za Kitanzania dau ambalo ni kubwa hivyo anaendelea na mazungumzo na iwapo atafanikiwa basi anaweza kuondoka wakati wowote kwani ndiyo matarajio yake,” alisema mzee Msuva.

No comments:

Post a Comment