SIMBA YATOKA SARE YA BAO 1-1 NA WAALGERIA HUKO UTURUKI, SALAMBA ASAWAZISHA MVUA IKIVUNJA PAMBANO - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 2 August 2018

SIMBA YATOKA SARE YA BAO 1-1 NA WAALGERIA HUKO UTURUKI, SALAMBA ASAWAZISHA MVUA IKIVUNJA PAMBANONaomba upokee picha za mchezo wa jana wa Simba SC na Mouloudia Oujda uliopigwa katika kiwanja cha hoteli ya The Green Park kilichopo katika mji mdogo wa Kartepe hapa Kocael, Uturuki.


Simba imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mouloudia Oujda ya Algeria katika mechi ya kirafiki iliyopigwa mjini Kocael katika vilima vya Kartepe nchini Uturuki.

Mouloudia Oujda walitangulia kufunga baada ya mechi kwisha kwa sare ya bila bao katika dakika 45 zote za kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili, Mouloudia Oujda walianza kufunga bao katika dakika ya 55 lakini Simba wakasawazisha katika dakika ya 58 kupitia kwa Adam Salamba dakika ya 58.

Hata hivyo mechi hiyo haikumalizika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mwamuzi kuisimamisha katika dakika ya 61.

No comments:

Post a Comment