SIMBA WAFICHUA SIRI YA KUSHINDWA KUWAWAFUNGA NAMUNGO LINDI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

SIMBA WAFICHUA SIRI YA KUSHINDWA KUWAWAFUNGA NAMUNGO LINDI


Uongozi wa klabu ya Simba umefichua siri ya kushindwa kuwafunga Namungo FC ya Ruangwa, Lindi baada ya kwenda nayo suluhu ya 0-0.

Simba walikuwa na mchezo wa kirafiki siku mbili zilizopita dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja wa Majaliwa uliopo mjini Ruangwa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari Simba, Haji Manara, amesema waliamua kutowafunga Namungo ili kuweka heshima kutokana mwaliko wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Majaliwa aliwaalika Simba ili wakacheze na Namungo kwa ajili ya uzinduzi hivyo Manara ameeleza ilibidi watumie busasara ili wasiweze kuleta aibu kwa Waziri.

"Tuliamua kutowafunga Namungo kwa ajili ya heshima ya Waziri, hauwezi kumwaibisha mtu mkubwa kama yule mwenye heshima zake" alisema.

No comments:

Post a Comment