SIMBA KUKWEA PIPA LEO KWENDA MWANZA KUFUATA NGAO YA HISANI - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 17 August 2018

SIMBA KUKWEA PIPA LEO KWENDA MWANZA KUFUATA NGAO YA HISANI

Na George Mganga

Kikosi cha Simba kinakwea pipa leo kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugari utakaopigwa kesho Agosti 18.

Simba itacheza na Mtibwa majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambao ukarabati wake umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 tayari kwa kipute kupigwa.

Simba ambao ni mabingwa wapya baada wa Ligi Kuu Bara baada ya kuukosa kwa takribani misimu mitano, wamesema wamejipanga kuhakikisha wanatwaa Ngao hiyo ili kuweka heshima.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, ameeleza kuwa wanakwenda Mwanza kuwapa furaha mashabiki na wanachama waliopo huko huku akisema hawawezi kuidharau Mtibwa hata kidogo.

Wekundu hao wa Msimbazi walipata tiketi ya kucheza mchezo huo baada ya kutwaa taji la ligi huku Mtibwa nao wakibeba kombe la FA baada ya kuilaza Singida United kwa mabao 3-2.

No comments:

Post a Comment