SERENGETI BOYS YAINYOA SUDAN 5-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KUWANIA KUCHEZA AFCON - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 16 August 2018

SERENGETI BOYS YAINYOA SUDAN 5-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KUWANIA KUCHEZA AFCON
Ukisema mambo safi utakuwa haujakosea baada ya timu ya taifa ya vijana ya chini ya miaka 17 kushinda kwa mabao 5-0 dhidi ya Sudan.

Serengeti Boys imeangusha kipigo hicho maridadi dhidi ya Sudan katika  michuano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kwa ushindi huo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Serengeti Boys imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.


Ushindi huo mnono wa mabao matano, unaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi sita baada ya mechi mbili na kupanda kileleni, Rwanda yenye pointi sita imeporomoka, huku Serengeti ikisaidiwa na wastani wao mzuri wa mabao.

No comments:

Post a Comment