Samatta afanya yake KRC Genk ikichomoza na ushindi dhidi ya Lech Poznan - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Samatta afanya yake KRC Genk ikichomoza na ushindi dhidi ya Lech Poznan

Nahodha wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ameisaidia timu yake kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0  dhidi ya Lech Poznan mzunguko wa tatu Europa league.
Mchezo huo uliyopigwa hapo jana kwenye uwanja wa Luminus Arena (Genk), Samatta aliweza kufunga bao lapili kupitia mpira wa kichwa dakika ya 56 kipindi cha pili huku goli lakwanza likiwekwa kimyani na mchezaji mwenzake, Ruslan Malinovsky dakika ya 44 kabla ya mapumziko.
Siku za hivi karibuni, Samatta amehusishwa na kuhamia ligi kuu ya Hispania La Liga kutokana na klabu kadhaa kuhitaji huduma yake ikiwemo Levante wakati waajiri wake KRC Genk ikikataa ofa ya euro milioni nane.

No comments:

Post a Comment