Rushwa yamtia Kifungoni Miaka Miwili Kalusha Bwalya - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 11 August 2018

Rushwa yamtia Kifungoni Miaka Miwili Kalusha BwalyaFifa imebaini gwiji la soka Zambia, Kalusha Bwalya alihusika na kuchukua rushwa kutoka kwa kiongozi wa Qatar, Mohammed Bin Hamman. 

Hivyo imemfungia kujihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka miwili. 

Bwalya ni gwiji la soka nchini Zambia na alikuwa kati ya watu waliokuwa wakituhumiwa katika sakata hilo lililochukua muda mrefu. 

Imeelezwa mwaka 2009, Bwalya alipewa kitita cha dola 50,000 kutoka kwa Bin Hamman na mwaka 2011 akaongezewa nyingine dola 30,000 ili amchague kiongozi huyo wakati akigombea uongozi, nafasi ya Rais wa Fifa dhidi ya Sepp Blatter.

No comments:

Post a Comment