Rais Magufuli Ashusha Matrekta 10 chuo cha SUA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 12 August 2018

Rais Magufuli Ashusha Matrekta 10 chuo cha SUA

Rais Dk John Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kutoa matrekta 10 kwa Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo - SUA- ili kuimarisha utoaji wa mafunzo ya kilimo na kutoa wataalamu bora wa kilimo nchini.

Matrekta hayo 10 aina ya Ursus yamekabidhiwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Kibaha Mkoani Pwani na kueleza kuwa SUA imepatiwa matrekta hayo ikiwa ni juhudi za Serikali za kuendeleza kilimo ambacho kinatoa ajira kwa Watanzania wengi.

Matrekta hayo yana thamani ya Shilingi Milioni 587.5

Dotto amekitaka Chuo Kikuu cha SUA kuyatumia matrekta hayo vizuri na kwamba Serikali itafuatilia kupitia kitengo cha Wizara ya Fedha na Mipango cha kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo katika taasisi ambayo inapokea fedha za Serikali.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SUA Profesa Yonika Ngaga amemshukuru Rais MAGUFULi kwa kutekeleza ahadi hiyo pamoja na kutekeleza ahadi ya kujenga mabweni ya chuo, ambapo SUA imepokea Shilingi BILIONI mbili na kuahidi kuwa chuo kitajiimarisha zaidi katika utoaji taaluma bora ya kilimo inayoendana na wakati wa sasa.

No comments:

Post a Comment