Polisi washauri mbwa wavalishwe viatu - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 6 August 2018

Polisi washauri mbwa wavalishwe viatu

Polisi katika mji wa Zurich nchini Uswisi wamewashauri wananchi wake kuwanunulia mbwa wao viatu ili kuwakinga na athari za viwango vya juu vya joto vinavyowatesa sasa wakazi wa bara la Ulaya.
Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Kitaifa (SRF), Polisi mjini Zurich wamezindua kampeni ya kuwapa ushauri wafugaji wa mbwa, jinsi ya kuwakinga wanyama wao kutokana na joto la juu.
Hatua hiyo imekuja baada ya hali hiyo ya joto, kusababisha barabara na baraza kushika joto linaloathiri hata watembea kwa miguu wakiwemo mbwa ambao hawavai chochote kuwakinga na athari hizo.
Kiwango cha juu sana cha joto kimeshuhudiwa msimu huu katika bara la Ulaya, huku Uswizi ikishuhudia kiwango cha juu zaidi cha joto kutokea tangu mwaka 1864.
Kiwango cha joto mwezi Julai kilifikia nyuzi 30.
Kulingana na msemaji wa polisi Michael Walker, nyuzi 30 ni sawa na kati ya nyuzi 50-55 ardhini au kwenye lami kutokana na ukweli kwamba ardhi huhifadhi joto zaidi.

No comments:

Post a Comment