Polisi Mkoani Kigoma Imekamata Silaha ya Kivita Aina ya AK47 - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 13 August 2018

Polisi Mkoani Kigoma Imekamata Silaha ya Kivita Aina ya AK47

Polisi mkoani Kigoma imekamata silaha ya kivita aina ya AK47 katika tukio la ujambazi ambalo lilisababisha vifo vya watu wanne.

Katika tukio hilo lililotokea Ijumaa iliyopita, polisi waliwaua watu watatu walipokuwa katika msako wa kuwasaka watuhumiwa wa ujambazi waliomuua Lukas Luchapa (38), saa tano usiku katika Kijiji cha Kigina, Kibondo.

Mbali ya kuwa na silaha hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno alisema jana katika tukio hilo walikamata pia risasi 69 na magazine tatu kwamba bunduki hiyo ina usajili wa Burundi.

Alisema watu hao walimuua Luchapa kwa kutumia silaha hiyo walipomvamia akiwa ametoka kunywa pombe.

Alisema awali, walitaka kuweka magogo barabarani kuzuia magari kabla ya mtu huyo akiwa ameonekana kama amepotea njia kutokea na kuanza kumshambulia kwa risasi za kichwani na mguuni.

“Tulipata taarifa hizo kwa kushirikiana na wananchi wa kijijini na tulifuatilia na kugundua walikuwa watu kama saba,” alisema Kamanda Ottieno.

Alisema askari wake walianza kuwasaka watu hao na kukutana nao katika msitu ulio karibu na kijiji hicho na kuanza majibizano ya risasi.

Alidai kwamba mmoja wa watuhumiwa hao aliuawa alipokuwa akijaribu kuwashambulia polisi kwa risasi.

Kamanda Ottieno alisema msako unaendelea kuwatafuta watu wanne waliokimbia kwa kuwasiliana na nchi jirani ya Burundi.

“Niwaombe wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kutoa taarifa pale wanapomuona mtu mgeni na kumtilia shaka kijijini,” alisema Ottieno.

No comments:

Post a Comment