POGBA, MOURINHO, GERVINHO, OSPINA, DE BRUYNE: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 16 August 2018

POGBA, MOURINHO, GERVINHO, OSPINA, DE BRUYNE: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS


Kiungo wa kati mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne kutoka Ubelgiji mwenye miaka 27 anatarajiwa kutocheza kwa miezi mitatu baada ya kuumia kwenye kano za goti la kulia. (Mirror)

Baadhi wanatarajiwa De Bruyne hataweza kucheza kwa miezi miwili hadi minne kutokana na jeraha hilo lake la goti. (Telegraph)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alimwambia Paul Pogba anafaa kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka iwapo hataki kusalia katika klabu hiyo. Mfaransa huyo mwenye miaka 25 naye amemjibu Mreno huyo kwa kumwambia kwamba atawasiliana naye kupitia kwa wakala wake pekee. (Sun)

Bayern Munich wanamnyatia beki wa Tottenham mwenye miaka 29 anayetokea Ubelgiji Toby Alderweireld. (Mirror)

Kipa wa Arsenal mwenye miaka 29 kutoka Colombia David Ospina amejiunga na Napoli kwa mkopo. (Guardian)

Parma wanakaribia kumnunua mshambuliaji wa Ivory Coast mwenye miaka 31 Gervinho kutoka klabu ya Hebei Fortune ya China wanapojiandaa kurejea kucheza katika Serie A. (Mediaset - in Italian)

Liverpool wamekataa ofa kutoka kwa Torino ambao wamekuwa wakimtaka kiungo wa kati wa Serbia mwenye miaka 22 Marko Grujic. Klabu hiyo ya Italia ilikuwa inamtaka mchezaji huyo kwa mkopo wa msimu mmoja na uwezekano wa kumnunua kikamilifu kwa bei ya £9m mwaka ujao. (Liverpool Echo)

Klabu ya Sydney FC ya Australia inafanya mazungumzo na mshambuliaji wa England mwenye miaka 31 Adam Le Fondre. Mchezaji huyo hana mkataba wowote baada yake kuondoka Bolton Jumanne. (Fox).

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment