POGBA, COURTOIS, BOATENG, MANCHESTER, CHELSEA: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 8 August 2018

POGBA, COURTOIS, BOATENG, MANCHESTER, CHELSEA: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO


Kiungo wa kati wa Machester United raia wa Ufaransa Paul Pogba amewaaambia wachezaji wenzake kuwa anataka kuhama Old Trafford na kujiunga na Barcelona.

United wamekosa kumsaini mlinzi wa Bayern Munich Jerome Boateng. Mlinzi huyo Mjerumani alimpigia simu meneja wa United Jose Mourinho kumuambia kuwa ameshukuru kwa nia hiyo lakini hawezi akaelekea Machester. (Bild)

Hata hivyo Leicester City wameipa United Matumaini mapya ya kumsaini mlinzi raia wa England Harry Maguire, 25, baada ya kuwaweka kwenye ofa walininzi wawili. Raia wa Crotaia Filip Benkovic, 21 alifanyiwa uchunguzi wa kiafya kablaa ya makubaliano yake ya pauni milion 13.5 kutoka Dainamo Zagreb na mkataba wa paunia milioni 22.5 kwa mchezaji wa Freiburg raia wa Uturuki Caglar Soyuncu, 22, unakaribia. (Mirror)

Kipa wa Athletic Bilbao Kepa, ambaye anakaribia kujiunga na Chelsea kwa paunia milioni 71.5 nusura ajiunga na Real Madrid kwa pauni milioni 17.9. Mlinda lango huyo raia wa Uhispania atakuwa kipa ghali zaidi wakati atahamia huko Stamford Bridge. (Guardian)

Kepa anasafiri kwenda London kukamilisha kuhama kwake kwenda Chelsea hatua ambayo itamuongezea mshahara wake wa sasa wa euro milioni kwa mwaka. (AS)

Atachukua mahala pake Mblegiji Thibaut Courtois ambaye anaamini kuwa kukataa kwake kurejea Chelsea kufanya mazoezi kutalipwa na kuhamia Real Madrid. Klabu hiyo ya Uhispnaia unajiandaa kumruhusu kiungo wa kati raia wa Croatia Mateo Kovacic, 24, kuelekea Stanford Bridge kwa mkopo kama sehemu ya mkataba huo. (Daily Telegraph)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment