Pogba Awapa Taarifa Wachezaji wenzake wa Old Trafford Nia Yake ya Kujiunga na Barcelona - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 8 August 2018

Pogba Awapa Taarifa Wachezaji wenzake wa Old Trafford Nia Yake ya Kujiunga na Barcelona

Kiungo wa kati wa klabu ya Machester United na raia wa Ufaransa Paul Pogba amewaaambia watu wake wa karibu pamoja na wachezaji wenzake kuwa anataka kuondoka Old Trafford na kujiunga na wababe wa Katalunya FC Barcelona.Mfaransa huyo amekuwa na wakati mgumu katika klabu hiyo kwani msimu uliopita ilisemekana hawana uelewano mzuri na kocha wake Jose Mourinho,huenda ndo ikawa sababu ya kiungo huyo kutaka kuachana na Mourinho.

Lakini pia Pogba amekuwa na ukaribu na beki wa kati wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Barcelona Umtiti kwani baada ya michuano ya kombe la Dunia kumalizika walionekana wakiwa wote nchini Marekana wakiwa mapumzikoni.Licha ya kiungo huyo kutaka kuondoka Old Trafford,Manchester United walihusishwa katika usajili wa wachezaji kadhaa wakiwemo mabeki wa kati wa klabu za Leicester ambaye ni Henry Maguire,beki wa klabu ya Tottenham Toby Alderweireld pamoja na beki wa Bayern Munich Jerome Boateng,kwa taarifa za sasa hivi asubuhi beki huyo tayari amemjibu Mourinho kuwa hayuko tayari kuhama Bayern na kujiunga na Manchester.


SAINT PETERSBURG, RUSSIA – JULY 10: Paul Pogba of France arrives at the stadium prior to the 2018 FIFA World Cup Russia Semi Final match between Belgium and France at Saint Petersburg Stadium on July 10, 2018 in Saint Petersburg, Russia. (Photo by Michael Regan – FIFA/FIFA via Getty Images)
Pogba alisajili na Manchester United kutoka Juventus kwa ada ya uhamisho wa Euro Mil 89,ikiwa ndio rekodi ya timu kununua mchezaji kwa gharama kubwa.

No comments:

Post a Comment