Mzee Majuto Asimamisha Shughuli Tanga Mamia ya Watu Wajitokeza Kumzika - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Mzee Majuto Asimamisha Shughuli Tanga Mamia ya Watu Wajitokeza Kumzika

Maelfu wamejitokeza kuusindikiza Mwili wa msanii Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto kuelekea Msikitini kabla ya kwenda eneo alilochagua kuzikwa.

Mzee Majuto alifariki usiku wa Jumatano, Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Muhimbili, ambapo kesho yake, Agosti 9, 2018 mwili wake ulipelekwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga, jijini Dar es Salaam, kuswaliwa kabla ya kupelekwa viwanja vya ukumbi wa Karimjee kuagwa. Baadaye mwili huo ulisafirishwa kuelekea jijini Tanga kwa maziko.


No comments:

Post a Comment