Mzee King Majuto azikwa Tanga - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Mzee King Majuto azikwa Tanga


Hatimaye mwili wa muigizaji wa vichekesho Amri Athumani maarufu kama Mzee King Majuto umehifadhiwa nyumbao kwake huko Donge, Tanga nchini Tanzania.

Kabla ya kuhifadhiwa wmili huo ulisafirishwa jana usiku hadi Tanga ambapo ulisimamishwa njiani kuwapa mashabiki fursaya kutoa heshima zao za mwisho.

Dua ya kuaga mwili wa marehemu huyo aliyefariki Jumatano usiku akitibiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ilifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Leo ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza mwendo wa saa sita mchana katika msikiti wa Nuruguda uliopo karibu na nyumbani kwake.

Baadaye mwili wake utazikwa kijiji cha Kiruku yalipo mashamba yake nje kidogo ya jiji la Tanga.

kiwa kama mfalme wa tasnia ya maigizo ya uchekeshaji nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mzee Majuto aliweza kujizolea umaarufu mkubwa kupitia namna ambavyo alikua akiigiza na kuwa miongoni mwa watu wenye mvuto mkubwa miongoni mwa wasanii.

Afya ya Mzee Majuto ilizorota zaidi mwanzoni mwa mwaka 2018 ambapo awali alipelekwa nchini India kwa matibabu baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli na wapenzi wa sanaa ya Mzee Majuto kumchangia ili kunusuru uhai wake kabla ya baadae kurejea nchini Tanzania.

Awali alidaiwa kuugua ugonjwa wa henia na baadaye tezi dume.

No comments:

Post a Comment