Mwalimu afumaniwa akimfanyia mwanafunzi mtihani - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 11 August 2018

Mwalimu afumaniwa akimfanyia mwanafunzi mtihani

Mwalimu mkuu wa shule nchini Burundi amekamatwa kwa kudanganya kuwa yeye ni mwanafunzi akiwa na lengo la kumfanyia mtihani mtu mwingine.

Polisi waliingia kwenye ukumbi wa mtihani ambapo Benjamin Manirambona alikuwa akifanya mtihani huo.

Hakufahamu kuwa polisi ambao walikuwa wamevalia nguo za raia walikuwa waemsubiri usiku kucha shuleni ili wamkamate.

Bila ya kuwepo mahala pa kutorokea mwalimu huyo mkuu wa taasisi ya Butere alikiri papo hapo.

Rais Buhari aunga mkono kufutwa walimu 20,000 kwa kufeli mitihani
Bw Manirambona alieleza kuwa alikuwa akifanya mtihani huo wa niaba ya mwanajeshi aliyekuwa akihudumu nchini Somalia kama sehemu ya kikosi cha Burundi cha kulinda amani. Alisema mwanafunzi alihitaji alama hizo hizo ili apate kujiunga na chuo kikuu.

Mwalimu huyo mkuu alisema mwanajeshi huyo alimuahidi kumlipa mara atakaporudi Burundi.

Alikamatwa pamoja na wanafunzi wengine wanne ambao pia walishukiwa kudanganya

"Kila kitu unachosema na uwongo, kwa hivyo tunakuchukua," alisema waziri wa elimu nchini Burundi Janvière Ndirahisha, ambaye aliwasili na polisi eneo kisa hicho kilitokea mjini Bujumbura.

"Tutachunguza kwa sababu kulingana na habari ambazo tumepata sio mara ya kwanza unafanya kitendo kama hiki," alimuaabia Bw Manirambona.

Alikamatwa pamoja na wanafunzi wengine wanne ambao pia walishukiwa kudanganya mmoja akilaumiwa kwa kuwaunganisha mwanajeshi na mwalimu huyo.

Bw Manirambona sasa yuko kwenye kizuizi cha polisi.

Nchini Burundi wanafunizi wanaofanya mitihani muhimu hupelekwa kufanyia shule zingine na ndiyo sababu Bw Manirambona hakuweza kutambuliwa na watu kwenye ukumbi wa mtihani.

No comments:

Post a Comment