Msafara wa Mzee Majuto Wasimamishwa vijiji 14 Ili Mashabiki Wake Kutoa Hshima ya Mwisho - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

Msafara wa Mzee Majuto Wasimamishwa vijiji 14 Ili Mashabiki Wake Kutoa Hshima ya Mwisho

Mwili wa muigizaji wa vichekesho Amri Athumani 'Mzee Majuto' umewasili Donge nyumbani kwake  jana 7.05 usiku baada ya kusimamishwa katika vijiji 14 na mashabiki wakitaka kutoa heshima ya mwisho.

Safari ya kwenda Tanga kwaajili ya mazishi ilianza saa 10.15 jioni baada ya kumuaga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Leo kuanzia saa 5.45 mchana, ibada ya mazishi itafanyika katika msikiti wa Nuruguda uliopo karibu na nyumbani kwake na kuzikwa kijiji cha Kiruku yalipo mashamba yake nje kidogo cha jiji la Tanga.

Mwili ulipowasili nyumbani kwa Mzee Majuto, kuliibuka vilio huku wanawake wengi wakizimia.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja jina la Mzee Majuto lilitawala vyombo vya habari likihusishwa na ugonjwa wa henia na baadaye tezi dume.

Januari mwaka huu, Mzee majuto alifanyiwa upasuaji wa tezi dume katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, kidonda cha upasuaji wa henia kiliendelea kumsumbua na alilazwa kwa mara nyingine katika hospitali hiyo katikati ya mwezi Aprili.

Mei 4, mwaka huu Mzee Majuto alisafirishwa kwenda India kupata matibabu katika hospitali ya Apollo, katika Jiji la New Delhi.

June 23, mwaka huu Mzee Majuto alirejea nchini baada ya kupata matibabu yaliyokuwa yakigharamiwa na Serikali na moja kwa moja alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya uangalizi kabla ya kuruhusiwa na kisha kurudishwa tena Julai 31 hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment