MOURINHO AWAPA TAHADHARI MANCHESTER UNITED - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 6 August 2018

MOURINHO AWAPA TAHADHARI MANCHESTER UNITED


Manchester United watakabiliwa na "msimu mgumu" iwapo hawataimarisha kikosi chao kwa kuwanunue wachezaji wapya kabla ya kipindi cha kuhama wachezaji kufungwa Alhamisi.

Hii ni baada ya Mashetani Wekundu kukamilisha mechi za kirafiki za kujiandaa kwa msimu mpya kwa kuchapwa 1-0 na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich siku ya Jumapili.

Javi Martinez alifunga kwa kichwa bao pekee katika mechi hiyo ambayo Bayern waliitawala.

"Afisa Mkuu Mtendaji wangu (wa Man Utd) anafahamu ninataka nini na bado nina siku kadha za kusubiri na kuona nini kitatokea," Mourinho alisema akizungumza na runinga ya klabu hiyo MUTV.

"Klabu hizo nyingine zinazoshindana nasi zina nguvu sana, zimejiimarisha sana na tayari zina vikosi vizuri sana. Au wanawekeza sana kwa mfano Liverpool, ambao wananunua kila kitu na kila mtu.

"Tusipoboresha kikosi chetu basi utakuwa msimu mgumu sana kwetu."

United kufikia sasa wamewanunua wachezaji watatu tu kipindi cha sasa cha kuhama wachezaji.

Kwa mujibu wa BBC, Wachezaji hao ni kiungo wa kati Mbrazil Fred aliyewagharimu £47m, beki Mreno Diogo Dalot na kipa nambari tatu Lee Grant.

Wataanza kampeni yao Ligi ya Premia kwa mechi dhidi ya Leicester City uwanjani Old Trafford Ijumaa.

Afisa mkuu mtendaji wa zamani wa United Peter Kenyon alisema Jumapili kwamba Mourinho anafaa kutafuta njia ya "kutatua" mzozo wake na naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward.

No comments:

Post a Comment