Mourinho aamua kuacha kufikiria usajili ‘muda umefika wa mimi kuacha kufikiria hili’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 9 August 2018

Mourinho aamua kuacha kufikiria usajili ‘muda umefika wa mimi kuacha kufikiria hili’

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa hana uhakika wa kufanya usajili mwingine kabla ya dirisha la usajili halijafungwa saa chache zijazo
Mourinho amekuwa akihitaji kumsajili beki wa kati wa Leicester City, Harry Maguire,  Toby Alderweireld  anayekipiga Tottenham Hotspur na Jerome Boateng  ili kuimarisha safu yake ya ulinzi.
Lakini meneja huyo raia wa Ureno kupitia mkutano wake na waandishi wa habari mapema hii leo ameeleza kuwa kunauwezekano mkubwa wa kutoongeza mchezaji mwingine ndani ya kikosi chake kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili leo siku ya Alhamisi.
Sina uhakika wa kuongeza mchezaji mwingine kabla ya dirisha hili la usajili halijafungwa leo hivyo ni muda kwangu kuacha kufikiria swala hilo.
Nitajaribu kuwa bize na wachezaji niliyonao katika michezo mitatu iliyopita kwasababu baada ya mechi na Spurs tutakuwa na mapumziko ya wiki kadhaa hivyo nitatumia muda huo kuwafanya wanaimarika.
Habari niliyonayo nikuwa hakuna usajili mwingine hivyo nitalazimika kuwa bize na wachezaji waliyopo kwa sasa.
Wachezaji kama Sergio Romero, Antonio Valencia, Marcos Rojo, Dalot, Ander Herrera na Nemanja Matic hawatakuwepo kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu Uingereza hapo kesho siku ya Ijumaa. Wakati huo huo Mourinho atalazimika kutazama ‘fitness’ ya wachezaji wake waliyochelewa kujiunga na kikosi baada ya kuwa mapumziko kutokana na kuzitumikia timu zao za taifa kwenye michuano ya kombe la dunia Urusi.

No comments:

Post a Comment