Mkemi awataka Yanga wamshukuru Nchemba - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 2 August 2018

Mkemi awataka Yanga wamshukuru Nchemba


Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ndani ya Yanga, Salum Mkemi, amefunguka kuhusiana na Yanga kutamba kuwa wamefanya usajili kwa baadhi ya wachezaji na kusahau kuwa Mwigulu Nchemba aliwapa msaada.

Kwa mujibu wa Radio One, Mkemi ameeleza kuwa ni vema Yanga wakamshukuru kutokana na msaada wake, Nchemba ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini huku akiwa ni Mlezi wa Singida United FC.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika kuibuka siku moja baada ya dirisha la usajili kufungwa na kueleza kuwa hakuna mchezaji yoyote ambaye walisaidiwa zaidi ya wao wenyewe.

Kutokana na kauli hiyo, Mkemi amesema Yanga wanapaswa walau kusema Ahsante kwa kitendo cha Nchemba kuwapa msaada wa wachezaji kadhaa kwasababu klabu imekuwa inapitia kipindi kigumu zaidi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, hivi karibuni aliibuka na kusema Nchemba alifanya mchakato wa kuwasaidia Yanga beki ambaye walipaswa kumsajili kutoka JKU, Feisal Salum 'Fei Toto' pamoja na Deus Kaseke kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao.

No comments:

Post a Comment