MH:JOKATE AZUNGUNZA NA WATUMISHI WA KISARAWE - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 8 August 2018

MH:JOKATE AZUNGUNZA NA WATUMISHI WA KISARAWE

Mhe. Jokate :Nidhamu,Bidii,Ushirikiano  Vitaijenga Kisarawe

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia,  Mkuu wa Wilaya mpya wa Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amekutana na watumishi wa Wilaya ya Kisarawe kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

Kutaniko hilo limefanyika siku ya jumatatu ambapo lengo kubwa likiwa ni  kutambulishana ,kufahamiana na kuweka mikakati jinsi ya kuwahudumia wananchi katika kuleta maendeleo yao na  Wilaya kwa ujumla

Awali  wakati anamkaribisha  Mkuu wa Wilaya azungumze na watumishi ,Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Ndugu Mtela Mwampamba aliwatambulisha watumishi hao mbele ya Mkuu wa Wilaya kwa kutambulisha watumishi hao kwa kila idara na vitengo na kueleza kwa kifupi matarajio ya watumishi kwa ujio wa mkuu a wilaya mpya

Akihutbia kutaniko hilo Mkuu wa Wilaya alianza kwa kujitambulisha na kuelezea matumaini makubwa ya ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu katika kuwahudumia wananchi wa kisarawe na kuwaletea maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye utekelezaji wa mipango ya serikalia inaytekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

Aidha Mkuu wa Wilaya huyo  amebainisha  mambo makuu matatu ambayo kwa pamoja yakifuatwa yataleta tija kubwa kwenye kuleta maendeleo kwa wananchi

‘’  lengo kuu la kukuatana hapa ni kufahamiana na kuwekana sawa na tutakuwa watumishi wa mfano bora na wa kuigwa .Mkusayiko huu unaashiria vitu vingi,unaashiria mshikamano.ili tusonge mbele tunahitaji kuwa na nidhamu ya kazi, bidii na ushirikiano’’ amesema mheshimiwa Jokate Mwegelo

Kaimu  mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu Patric Allute amesema wanamkaribisha na watumishi wamemsikiliza na watatekeleza maaagizo yote ili kuweza kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.

Mheshimiwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amefanikiwa kukutana na watumishi.
Na Mwandishi Wetu

No comments:

Post a Comment