Meli ya Mizigo Yateketea kwa Moto Bagamoyo - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

Meli ya Mizigo Yateketea kwa Moto Bagamoyo

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutaja chanzo chake kuwa ni hitilafu ya umeme wakati mafundi wakijaribu kuchomelea mlango wa meli hiyo kwa kutumia umeme wa jenereta iliyokuwa ndani yake.

Amesema vyombo vya zimamoto na uokoaji vimefanikiwa kuzima moto huo na kwamba nahodha kwa sasa anahojiwa na vyombo vya usalama ii kupata maelezo zaidi.

Inadaiwa kuwa meli hiyo imetokea visiwani Zanzibar na ilikuwa bandarini hapo ikisubiri shehena ya kokoto kwa ajili ya kuipeleka Zanzibar.

No comments:

Post a Comment