MDHAMINI MKUU LIGI KUU BARA AWEKWA HADHARANI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

MDHAMINI MKUU LIGI KUU BARA AWEKWA HADHARANI


Na George Mganga 

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) limesema kuwa leo litamuweka hadharani Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara zikiwa zimesalia siku chache pazia kufunguliwa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema mdhamini huyo watamtangaza leo baada ya kufikia nao mwafaka.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita TFF wakingie mkataba na Bank ya KCB ulio na thamani ya kiasi cha milioni 420 wakiwa kama wadhamini washiriki.

Hivi karibuni TFF walisema walikuwa katika mazungumzo na wadhamini wakuu ambao ni Kampuni ya Mawasiliano, Vodacom japo hawakuweza wazi wamefikia hatua ipi.

Wakati TFF wakisubiriwa kumtangaza mdhamini, pazia la michuano ya Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao litaanza Agosti 22 2018.

No comments:

Post a Comment