MCHAKATO WA UCHAGUZI YANGA KUMPATA MBADALA WA MANJI KUANZA LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 15 August 2018

MCHAKATO WA UCHAGUZI YANGA KUMPATA MBADALA WA MANJI KUANZA LEO


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema leo ndiyo siku ya kuanza mchakato rasmi wa uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi ambazo zipo wazi mpaka sasa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa siku 75 za klabu hiyo pamoja na Simba kufanya uchaguzi ili kutimiza matakwa ya katiba zao.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Omary Kaaya, amesema wanalazima kuanza rasmi mchakato ili kuwapata viongozi muhimu ambao nafasi zao zipo wazi hadi sasa.

Nafasi hizo ni ya Mwenyekiti wa klabu, Makamu Mwenyekiti na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Wakati Yanga ikianza mchakato, kikosi cha timu hiyo kipo mjini Morogoro kuendelea na maandalizi ya kukabiliana na USM Alger kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.


Yanga leo itakuwa mjini Kilombero kucheza na timu ya daraja la pili, Mkamba Rangers kwa ajili ya kuwapa kipimo kizuri wachezaji wake kuelekea mechi hiyo kubwa Agosti 19.

No comments:

Post a Comment