MBELGIJI SIMBA KUANZA NA REKODI HII UNYAMANI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

MBELGIJI SIMBA KUANZA NA REKODI HII UNYAMANI


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameweka wazi kuwa, ataanza kuingia kwenye rekodi ya makocha waliopa timu hiyo mataji wakati atapochukua Ngao ya Jamii wiki hii watakapokutana na Mtibwa Sugar.

Mbelgiji huyo ambaye amechukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre, wikiendi hii ana kibarua kigumu cha kuiwezesha Simba kutwaa taji lake la kwanza kwa msimu huu wakati watakapopambana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Klabu hizo mbili zinakutana kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Kirumba, Mwanza baada ya Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu wakati Mtibwa wakiwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho (FA).

Mbelgiji huyo amesema kuwa anataka kushinda taji hilo la Ngao ya Jamii na wana uhakika mkubwa wa kushinda kutokana na ubora wa timu yake ambayo amekuwa akiipa mbinu kwa kadiri wanavyoenda kucheza mchezo huo.

“Ninataka kuanza na rekodi ya kutwaa mataji sasa na kombe pekee ambalo lipo mbele yetu ni Ngao ya Jamii. Ni lazima tushinde na kuchukua kombe hilo licha ya kuambiwa wapinzani wetu ni timu nzuri na wana ushindani.

“Niseme tu kwamba wasione kwamba tumeshindwa kupata matokeo kwenye mechi zetu mbili za kirafiki (Asante Kotoko na Namungo FC) basi ndiyo wakajua kwenye mechi hiyo tutakuwa hivyohivyo, niwaambie tu katika mchezo huo tutabadilika na kuwa watu wengine kabisa,” alisema Mbelgiji huyo.

No comments:

Post a Comment