" Mavoko hajaondoka bado ni mali ya WCB' Salam SK - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 16 August 2018

" Mavoko hajaondoka bado ni mali ya WCB' Salam SK


Meneja wa Lebo ya Wasafi, Salam SK amesema bado mkali wa Bongo Fleva, Rich Mavoko ni msanii ambaye anamilikiwa na lebo hiyo licha ya tetesi kuzagaa kwamba amejitoa na sasa anafanya kazi zake binafsi.

Kwa siku za hivi karibuni Hitmaker huyo wa Kokoro amekuwa akihusishwa kujiengua ndani ya lebo hiyo ambayo alisaini nayo mkataba mrefu mwaka 2016.

Sasa leo kupitia kipindi cha The Playlist, Salam amesema wao kama WCB waliitwa na Baraza la Sanaa nchini Basata kuhusu malalamiko ambayo yalipelekwa na msanii huyo kuhusu baadhi ya vipengele vya mkataba wao lakini hiyo haimaanishi amejiengua.

" Hata tunapoongea hivi sasa Mavoko ni msanii wetu, ishu ya kuondoa jina la Wasafi kwenye bio yake Instagram hata Lil Wayne aliwahi kuondoa kuwa yupo Cash Money but aliendelea kusimamiwa na lebo hiyo, ni vitu vya kawaida, bado ni msanii wetu na siyo vinginevyo.

" Hata yeye alipewa gari kama ambavyo Mbosso na Lava Lava wamepewa, halafu ishu ya gari ni kila msanii anachagua gari anayotaka afu anakuwa anakatwa kwenye makato yake," amefichua Salam.

No comments:

Post a Comment