MASHINE MPYA SIMBA, JEZI, MFUMO KUTAMBULISHWA SIMBA DAY LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 8 August 2018

MASHINE MPYA SIMBA, JEZI, MFUMO KUTAMBULISHWA SIMBA DAY LEO


Wakati tamasha kubwa la Simba Day likitarajia kufanyika leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa, unaambiwa wanachama na wapenzi wengi wa klabu hiyo wanasubiria utambulisho wa wachezaji wao wapya.

Katika tamasha hilo Simba itashuka kucheza na timu ya Asante Kotoko kutoka Ghana ambayo imewasili jana kwa ajili ya kusherehesha siku hii maalum ambayo Simba huitumia katika utambulisho wa wachezaji ambao watatumika msimu ujao.

Moja ya wachezaji ambao wanasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hiyo, ni pamoja na kiungo Clatous Chama aliyesajiliwa kutoka Dynamos FC ya Zambia.

Ukiachana na utambulisho wa Chama, mashabiki wa timu hiyo wanasubiria kuona mfumo upi ambao kocha mpya Mbelgiji, Patrick Aussems ataanza nao huko mbele baada ya kutumia 4-4-2 wakati kikosi kikiwa Uturuki kwa kambi ya wiki mbili.

Katika msimu uliopita, Simba ambayo ilikuwa chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre, ilikuwa ikianza na wachezaji watatu mbele ambao ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya wakati leo wanataka kuona wapi wataanza kutokana na kikosi kuwa na ingizo.

Unaambiwa shughulo nzima itaanza majira ya saa 6 leo mchana leo ambapo kikosi B cha Simba kitacheza dhidi ya Dodoma FC B kisha baadaye mechi ya wakubwa itashika hatamu. Unakosaje?

No comments:

Post a Comment