MANARA AWAKA JUU YA GAZETI LILIOANDIKA SIMBA ILICHEZA NA MADEREVA TAXI, ATANGAZA KUMSAKA ILI AMSHUGULIKIE VIZURI - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 6 August 2018

MANARA AWAKA JUU YA GAZETI LILIOANDIKA SIMBA ILICHEZA NA MADEREVA TAXI, ATANGAZA KUMSAKA ILI AMSHUGULIKIE VIZURI


Imeelezwa kuwa Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amewaka na kueleza masikitiko yake juu ya taarifa iliyochapishwa na gazeti moja hapa nchini likieleza kuwa Simba imecheza na Umoja wa Madereva Tax Uturuki.

Simba ilicheza mchezo huo wa mwisho wa kirafiki na timu ijulikanayo kwa jina la F.C.E Ksaifa ya Palestina na kuifunga jumla ya mabao 3-1.

Baada ya gazeti hilo kuchapisha taarifa hiyo likieleza kuwa Simba hawakucheza na timu hiyo, Manara ameahidi kula sahani moja na Mwandishi wa gazeti hilo akieleza taarifa iliyoandikwa ni ya uongo.

Ofisa huyo amezungumza hayo akiwa katika hali ya mwonekano wa hasira akisema anahitaji kumjua Mwandishi huyo ili aweze kumshughulia vizuri kutokana na kuudanganya umma juu ya upotoshaji wa taarifa hiyo.

Wakati Manara akiahidi kiapo cha kumalizana na Mwandishi wa gazeti hilo, kikosi cha Simba ambacho kilikuwa Uturuki kwa wiki mbili, kinatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es Salaam, tayari kwa tamasha la Simba Day ambalo watacheza dhidi ya Asante Kotokoto kutoka Ghana, Jumatano ya wiki hii.

No comments:

Post a Comment