Man United kumtangaza Mkurugenzi wa michezo - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 14 August 2018

Man United kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa kuwa mkurugenzi wa michezo

Klabu ya Man United iko katika mpango wa kumtangaza Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo baada ya klabu hiyo kushindwa kufanya vyema katika dirisha kubwa la usajili

Katika mchakato huyo naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward atashirikiana kocha Jose Mourinho kumpata Mkurugenzi huyo wa michezo.

Tayari majina matatu yanatajwa kuweza kupewa nafasi hiyo ambao ni Golikipa wa zamani wa timu hiyo muholanzi Edwin Van Der Sar

Pia yupo mkurugenzi wa michezo wa As Roma Muhispania Ramón Rodríguez Verdejo maarufu kama Monchi pamoja na Fabio Paratici

No comments:

Post a Comment