Man City yamkaribisha Unai Emery kwakipigo EPL - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 12 August 2018

Man City yamkaribisha Unai Emery kwakipigo EPL

Meneja mpya wa klabu ya Arsenal, Unai Emery ameshuhudia vijana wake wakikubali kipigo cha jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Manchester City katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates.
Mabingwa hao watetezi wa Epl walianza kupata bao lamapema dakika ya 14 kupitia kwa Raheem Sterling ambaye sasa anafikisha jumla ya magoli 50 kwenye ligi hiyo wakati bao lapili likifungwa na Bernardo Silva kunako dakika ya 64.
Emery ambaye huu ndiyo mchezo wake wakwanza toka kujiunga na the Gunners anatarajiwa kuifikisha timu hiyo kwenye levo nyingine kutoka pale alipopaacha Mzee Arsene Wenger.
Vikosi vya timu zote mbili Arsenal: Cech (5), Bellerin (6), Sokratis (5), Mustafi (5), Maitland-Niles (5), Guendouzi (5), Xhaka (5), Mkhitaryan (5), Ramsey (6), Ozil (6), Aubameyang (6).
Wachezaji waakiba : Lichtsteiner (6), Lacazette (5), Torreira (5).
Man City: Ederson (6), Walker (7), Stones (6), Laporte (6), Mendy (7), Silva (8), Fernandinho (6), Gundogan (6), Mahrez (6), Aguero (6), Sterling (8).
Wachezaji waakiba: De Bruyne (6), Jesus (5), Sane
Mchezaji bora wamchezo : Bernardo Silva

No comments:

Post a Comment