MAHAKAMA YATAKA HANS POPPE, MWENZAKE WAONDOLEWE KATIKA KESI YA KINA AVEVA - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 10 August 2018

MAHAKAMA YATAKA HANS POPPE, MWENZAKE WAONDOLEWE KATIKA KESI YA KINA AVEVA
Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, leo imetoa siku saba kwa Jamhuri kuwaondoa Zacharia Hans Poppe na Frank Lauwo katika kesi inayowakabiri viongozi wa Simba ili iweze kuendelea.

Amri hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam baada ya washitakiwa wa kesi ya utakatishaji fedha, MWenyekkiti wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kuhudhuria mahakamani hapo.

Hans Poppe na Lauwo waliongezwa katika kesi hiyo lakini hawakuwahi kupatikana, jambo lililofanya kesi hiyo isiendelee kusikilizwa.

Aveva na Kaburu walifika makamani hapo huku Aveva akionekana kutembea kwa tahadhari kubwa kama mtu ambaye alikuwa bado anaugua.

Wakati fulani, Aveva aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuwa mgonjwa kwa muda mrefu.

Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 17, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment