Lulu Diva; Kuondoka kwa Rich Mavoko WCB Sio Mwisho wa Penzi Letu - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 16 August 2018

Lulu Diva; Kuondoka kwa Rich Mavoko WCB Sio Mwisho wa Penzi Letu

MWANAMUZIKI wa kike anayekuja kwa kasi kwenye anga ya Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa kuondoka kwa mpenzi wake Richard Martin’ Rich Mavoko’ kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, siyo mwisho wa penzi lao hata kama kwa upande wake ataendelea kuwa kwenye lebo hiyo.

Akizun-gumza na Showbiz Xtra, Lulu alisema kuwa amek-utana na maswali ya wengi ambayo yame-fanya afahamu kwamba wanahofu na penzi lao kwamba linaweza kuwa ni mwisho kwa sababu uhusiano wao ulianza wote wakiwa wapo kwenye lebo hiyo, lakini wafahamu kwamba penzi lao haliwezi kukatishwa na WCB.

“Watu wanahofia kwamba nitaachana na Mavoko kwa sababu ya kutoka WCB, hilo ni jambo lisilowezekana kwani tunapendana kweli na penzi letu halishikiliwi na lebo,” alisema Lulu ambaye inasemekana ni mjamzito.

No comments:

Post a Comment